#dodoma
TARURA YAKABIDHIWA RASMI MIKOBA YA KAZI, YAONYWA KUJIHUSISHA NA RUSHWA.
Watendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (Tarura) wametakiwa kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii na weledi na kuonesha mabadiliko katika utekelezaji wa miradi ya ujenzi wa barabara.

Wito huo umetolewa na Katibu mkuu wa TAMISEMI Mhandisi Musa Lyomba Katika Ufunguzi wa kikao cha watendaji mbalimbali wa TARURA mkoani Dodoma chenye lengo la kutoa muongozo na maelekezo ya majukumu kwa watendaji wa taasisi hiyo ,ambapo amewataka kutumia utaalamu wao katika kufanya kazi za barabara kwa weledi na juhudi bila kutoa kisingizio chochote.

Mhandisi Lyomba amesema kuwa hawategemei kuona mfanyakazi wa TARURA ikilalamikiwa kwa vitendo vya Rushwa bali wanatakiwa kuonesha mabadiliko kwa kujituma katika utendaji wao.
Kwa upande wao watendaji waliohudhuria kikao hicho wakiwemo Wahandisi kutoka mikoa mbalimbali hapa nchini wamesema kuwa kuanzishwa kwa wakala wa barabara vijijini na Mijini (TARURA) Itawezesha kufanikisha uboreshaji wa barabara za manispaa pamoja na zile za vijijini na kuleta ufanisi wa mioundombinu.
.
Kikao hicho cha watendaji wa wakala wa barabara Vijijini na Mijini TARURA kimehudhuriwa na watendaji mbalimbali wakiwemo Waratibu wa mikoa 26,Mameneja wa Makao makuu 180, wahasibu 170,Wakaguzi wa ndani pamoja na wahandisi.

Comments
Post a Comment