Na Dodoma Fm
BAADA ya kushinda tuzo Mchezaji Bora wa Mwezi
Agosti wa Azam FC, beki Mghana Yakubu Mohammed amepania kufanya mambo makubwa
zaidi kuisaidia timu hiyo.
Yakubu ametwaa tuzo hiyo inayojulikana kama ‘NMB
Player of the Month’ ikidhaminiwa na wadhamini wakuu wa timu hiyo Benki ya NMB,
na anakuwa mchezaji wa kwanza wa Azam FC kuitwaa ikiwa imeanzishwa msimu huu.
Kwa upande wa timu ya vijana ya Azam FC (Azam FC
U-20) tuzo hiyo imekwenda kwa kiungo Twaha Ahmed, ambayo inadhaminiwa na
wadhamini namba mbili wa timu hiyo Maji safi ya Uhai Drinking Water ikijulikana
kama ‘Uhai Player of the Month’.
Tuzo hizo za kwanza za Azam FC, zilitolewa na
mgeni rasmi kwenye mchezo wetu wa jana dhidi ya Lipuli, Rais wa Shirikisho la
Soka Tanzania (TFF), Wallace Karia.
Akizungumza jana mjini Dar es Salaam, Yakubu
aliishukuru Azam FC kwa kuanzisha tuzo hiyo akidai inaongeza ushindani kikosini
pamoja na kujenga wasifu wa wachezaji (CV).
Comments
Post a Comment