Na Dodoma Fm
Klabu ya soka ya mbeya city inayoshiriki ligi
kuuu tanzania bara imeingia mkataba wa
awali wa msimu moja na kocha Nsanzurwimo
Ramadhan kutoka nchini burundi kwa ajili
kukinoa kikosi hicho.
Akizungumza kwa njia ya simu Afisa habari wa mbeya city shah Mjanja amebainisha kuwa kocha huyo kutoka nchini
burundi anataraija kujiunga na timu hiyo mkoani Shinyanga kwa ajili ya kujjiwinda michezo ya ligi kuu
soka tanzania bara inayoendelea hivi sasa.
Lakini pia amebainisha hali ya timu kwa ujumla na
maendeleo yake baada ya kupoteza mchezo wa hivi karibuni wa mzunguko wa nne wa
ligi kuu tanzania bara dhidi ya stand
united ya mkoani shinyanga.
Amesema kuwa baada ya kupoteza mchezo huo
wamepania kufanya vizuri katika mchezo unaofuta dhidi ya Mwadui ya mkoani shinyanga
Na Selemani Juma Kodima
Comments
Post a Comment