Serikali kupitia wizara ya afya nchini imeweka mfumo mpya wa kielekronic kwa ajili ya kutunza takwimu za vifo pamoja na wagonjwa katika hospitali zote ili kuepuka upotevu wa takwimu hizo.

Akizungumza na kituo hiki mganga mfawidhi kutoka hospitali ya rufaa mkoa wa Dodoma General Dokta Carorine Damiani amesema takwimu hizo ni muhimu kwa kila hospital nchini kuzitunza ambapo awali kulikuwa na changamoto kubwa ya utunzaji wa takwimu hizo ambazo zilikuwa zinatunzwa kwa njia ya analogia.
Dokta Carorine amesema kufuatia utafiti uliofanywa na taasisi ya utafiti wa vifo na magonjwa ya binadamu nchini ambao umefanywa katika hospitali 39 umebaini kutokufanya vizuri katika njia ya uhifadhi wa takwimu kwa kutumia mfumo wa analogia.
Ameongeza kuwa matumizi ya mfumo mpya ambao umewekwa na serikali wa kuhifadhi takwimu kwa njia ya kielectronic utasaidia kuondokana na changamoto zote ambazo zilikuwepo kipindi cha nyuma.
Comments
Post a Comment