Mkuu wa wilaya ya Chemba mkoani
Dodoma Simon Odunga amemcharaza viboko mzazi wa
mmoja wa watoto walioshambulia gari lake kwa mawe na kuvunja kioo.
Gari hilo lenye namba za usajili
STL 669 lilishambuliwa na watoto watatu katika barabara kuu ya Kondoa Dodoma
kwenye kijiji cha Paranga Chemba .
Baada ya watoto hao kushambulia
gari na kuvunja kioo Mkuu huyo wa Wilaya alisimamisha gari na kuamua
kuwakimbiza watoto hao lakini hakufanikiwa kuwakamata ndipo baadhi ya mashuhuda
wa tukio hilo walipomuelekeza wanapoishi na hatimae DC akafika katika moja ya
familia.
Mkuu huyo wa Wilaya walirushiana
maneno na mzazi wa mmoja wa watoto hao kwa kile kilichoelezwa kuwa ni baada ya
mzazi kukerwa na maswali aliyomuuliza DC juu ya malezi ya Mtoto wake huku DC
nae akikerwa na majibu ya mzazi ndipo
akachukua jukumu la kumchapa na kumsababishia majeruhi.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma
Lazaro Mambosasa amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema
amechukizwa na kitendo cha mkuu huyo wa wilaya kujichukulia sheria mkononi na
kubainisha kuwa mtoto aliyevunja kioo ni wa miaka 9 hivyo kisheria haruhusiwi
kushtakiwa popote.
Na Selemani Juma
Chanzo:Dodoma FM
Comments
Post a Comment