VYOMBO VYA DOLA VYATAKIWA KUTUMIA BUSARA KATIKA UTATUZI WA MIGOGORO.
Na Dodoma fm
Vyombo vya Dola vimetakiwa kuwa kipaumbele kwa kutumia nafasi zao katika kudumisha amani ya nchi hasa katika maandamano na migomo inayotokea ili kuepusha nchi kuingia katika machafuko yanayoweza kujitokeza.

Hayo yameelezwa na
Mchambuzi wa maswala ya kisiasa Bw. Denis Nachipyangu wakati akizungumza na
Taswira ya habari ambapo amesema kuwa mara nyingi machafuko yanatokea iwapo
vyombo vya dola vikitumia nguvu katika kutatua migogoro au maandamano hivyo ni
vyema vikatumia akili na busara ili kuepuka kutokea kwa machafuko ya nchi.
Bw. Nachipyangu amesema
kuwa maandamano mengi yamekuwa yakipelekea machafuko kutokana na kuwa baadhi ya
watu wamekuwa na mawazo tofauti juu ya matokeo ya maandamano hayo ambapo wengi
wao wamekuwa wakihofia kutokea kwa vurugu na machafuko.
Sanjari na hayo Bw.
Nachipyangu ametoa rai kwa Wananchi
pamoja na vyombo vya dola kutokukiuka haki za kikatiba katika kufuata taratibu
na sheria za nchi badala yake vinatakiwa kutoa ulinzi kwa Wananchi ili waweze
kuendelea kuwa na imani na vyombo hivyo.
Comments
Post a Comment