Shirika la umeme TANESCO mkoa wa Dodoma
limewaomba wananchi katika maeneo ya vijijini kujitokeza katika mikutano ambayo
inaandaliwa na shirika hilo kwa lengo la kutoa elimu juu ya athari zitokanazo
na matumizi mabaya ya miundombinu ya umeme.
Akizungumza na Dodoma FM Afisa mahusiano
TANESCO Mkoa wa Dodoma Bwana Innocent Lupenza amekiri kuwa wananchi walio wengi
wa maeneo ya vijijini hawana Elimu ya Kutosha juu ya matumizi sahihi ya umeme.
Kufuatia hali hiyo Bwana Lupenza amesema
kulingana na tafiti zao wamegundua kuwa changamoto kubwa ni wananchi kuweka makazi yao
karibu na miundombinu ya TANESCO jambo
ambalo ni hatari kwao.
Na
Benard Filbert Chanzo:Dodoma
FM Radio
Comments
Post a Comment