Skip to main content

STEVE NYERERE AINGILIA KATI MALUMBANO YA DIAMOND, ALLY KIBA NA OMMY DIMPOZI AOMBA WAYAMALIZE.

kupitia ukurasa wa instagram wa msanii wa filamu nchini Steven Nyerere ameandika maneno ambayo yanaonesha kukasirishwa na maneno ya wasanii wabongofleva nchini Diamond, Ally kiba na Ommydimpoz nakuwataka wasanii hao kutowahusisha  wazazi kwenye malumbano yao ambayo yanaendelea mitandaoni.

Image may contain: 2 people, people smiling, text and closeup
hii ni post aliyoituma.

NIMEKAA NIMEJIFIKIRIA NIMEONA NISEME KIDOGO, DUNIA MAMA ANA HESHIMA YAKE KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE, MAMA NI KIOO CHA FAMILY MAMA NI NGUZO YA FAMILY MAMA NI KIMBILIO LA FAMILY , TUNAWEZA KUKOSEA KOTE LAKINI SI KWA MAMA NDOMANA AMNA LAANA YA BABA ILA LANA YA MAMA IPO NA INAFANYA KAZI HARAKA KULIKO KITU CHOCHOTE, SIZANI KAMA TUNA ELIMISHA JAMII KUPITIA MATUSI YA KUZALILISHA WAZAZI, NYINYI NI KIOO CHA JAMII, LAZIMA MUWE NA KIFUA CHA KUBAKISHA MANENO , MIMI NILIZANI HIZI NGUVU MNAZOTUMIA MNGEWEKEZA KWENYE MZIKI WENU TUNGEFIKA MBALI SANA , MMEJIJENGEA HESHIMA NA MMELITAFUTA JINA KWA SHIDA , ILA MNASAHAU JINA HILO LINAWEZA POTEA KWA SEKUNDE, NAWASHAULI NA NAKUSHAULI WEWE UNAYEZARAU WAZAZI FUTA KAULI NA OMBA MSAMAHA KWA MASHABIKI ZAKO USUSANI KINA MAMA WOTE AMBAO NAAMINI NI MASHABIKI WAKO NA NDIO WALIOKUFANYA UKAFIKA HAPO, HATUKATAI NYINYI NI BINADAMU INAWEZEKANA MMEPISHANA KAULI ILA KWENYE KUPISHANA WEKENI AKIBA YA MANENO, KUNA KESHO HUJUI ATAKAYE KUSTILI, HAKIKA BUSARA ITUMIKE , YANI NINGEKUWA MIMI NDIO UMEMGUSA RITA WANGU IVO DOOOO, MJINGA HAJIBIWI, KICHAA HAKIMBIZWI , MWIZI SI RAFIKI, NANI KAMA MAMA, ESHIMA ITAWALE ASANTE BY #####UZALENDO KWANZA,
NINI MAONI YAKO.

Comments

Popular posts from this blog

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...