HALMASHAURI YA MANISPAA YA DODOMA KUAJIRI ASKARI MIGAMBO 30.
Na Dodoma fm
Kamati ya fedha na mipango katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kwa kauli moja imekubaliana kuajiri askari migambo wapatao 30 watakao gawanywa katika tarafa 4 za Manispaa ya Dodoma ili kudhibiti ujenzi holela.
Na Dodoma fm
Kamati ya fedha na mipango katika Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma kwa kauli moja imekubaliana kuajiri askari migambo wapatao 30 watakao gawanywa katika tarafa 4 za Manispaa ya Dodoma ili kudhibiti ujenzi holela.
Mkurugenzi wa Manispaa
ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi amewaambia waandishi wa habari kuwa lengo la kuajiri
migambo hao ni kuhakikisha wanadhibiti ujenzi holela ambao umekuwa ukiendelea
katika mji wa Dodoma ambao ndio kitovu cha Nchi.
Miongoni mwa mambo
mengine ambayo uongozi wa Manispaa ya Dodoma unaendelea kuyafanyia kazi ni
pamoja na kukamilisha ujenzi wa soko katika eneo la Makole litakalotumika kwa
shughuli zote za wamachinga ili kupunguza kero pamoja na msongamano wa
wafanyabiashara hao katika eneo moja.
Hata hivyo licha ya
kuwahamishia wamachinga wote katika soko la Makole Mkurugenzi wa Manispaa ya
Dodoma amesema ulinzi mkali utaimarishwa
katika maeneo ya barabara ili kudhibiti uzalishaji wa wamachinga wengine ndani
ya mji wa Dodoma.
Baadhi ya
wafanyabiashara maarufu kama wamachinga katika manispaa ya Dodoma licha ya
kupongeza jitihada hizo wamesema hatua hiyo itawarudisha nyuma kiuchumi
kutokana na wao kufanya biashara kwa kufuata maeneo yaliyo na mkuanyiko mkubwa
wa watu.
Comments
Post a Comment