Serikali imeshauriwa kufanya marekebisho kwenye vigezo vipya
ambavyo vimewekwa na bodi ya mkopo nchini
kwa wanafunzi wa elimu ya juu ili kumuwezesha kila mwanafunzi ambaye
anasifa za kuendelea na chuo kikuu.
Ushauri huo umetolewa na mhadhiri kutoka chuo kikuu cha
Dodoma bwana Paul Luisulie wakati akiongea na kituo hiki ambapo amesema kuna
haja kubwa ya serikali kufanya marekebisho kwenye vigezo hivyo ambavyo
vimewekwa na bodi ya mikopo ya elimu ya juu ili kuepusha kutengeneza matabaka
baina ya watanzania.
Aidha ameziomba serikali za wanafunzi wa elimu ya juu kufuatilia
suala hilo ili kuleta haki sawa kwa kila mwanafunzi ambaye anasifa za kujiunga
na chuo kikuu anastahili kupewa mkopo na
sio kuwatenganisha katika madaraja tofauti.
Hivi karibuni bodi ya mikopo ya elimu ya juu nchini
imetangaza vigezo vipya kwa wanafunzi ambao wanatarajiwa kujiunga na vyuo vikuu
kwa mwaka wa masomo 2017/2018.
Kwa upande wao wazazi mkoania hapa akiwepo bwana Paul
Dickluck pamoja na Juma Msamilo wamesema ni vyema serikali ingefanya
marekebisho vigezo ambavyo vimewekwa na bodi ya mikopo nchini ili kila
mwanafunzi mwenye sifa ya kujiunga na chuo kikuu apatiwe mkopo ili aweze
kunufaika na elimu hiyo.
Na Benard filbert
Comments
Post a Comment