Kutokana na changamoto inayokikabili kituo cha kutoa huduma
ya elimu kwa watoto wenye ulemavu wa akili na viongo katika kata ya Miyuji kituo hicho kimeziomba taasisi binafsi pamoja
na serikali kukisaidia mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula.

Akiongea na Taswira ya habari Muhudumu wa kituo cha Cheshire
Home Sister Teresia Kosmas amesema kuwa wanaziomba
taasisi mbalimbali kuweza kuviangalia vituo hivyo kutokana na kuwa vituo kama
hivyo vimekuwa vikisahaulika katika misaada swala ambalo linapelekea kukabiliwa
na ukosefu wa mahitaji mbalimbali ikiwemo chakula.
Sister Teresia amewataka wazazi kujishugulisha katika kumuelekeza mtoto
mwenye matatizo ya viungo au akili vitu vya msingi ikiwemo kazi ndogondogo ili aweze kujitegemea katika baadhi ya vitu na
si kumtelekeza kama wanavyofanya baadhi ya wazazi.
Kutokana na kuwepo kwa unyanyapaa kwa watoto wenye ulemavu
Sister Teresia ameiomba jamii kuachana na tabia hiyo badala yake wawaone kama
watoto wengine .
Na Phina Nimrod
Chanzo;Dodoma fm
Comments
Post a Comment