Watumiaji wa vyombo vya moto barabarani wakiwemo wamtembea kwa miguu wanatajwa kuwa wadau wakubwa katika kupinga na kutokomeza ajali za barabarani kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Afisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Dodoma Kopro Athuman Rashidi ameiambia Dodoma Fm kuwa matukio ya ajali za barabarani yanaweza kutokomezwa iwapo kila mwananchi atawajibika kwa nafasi yake.
Amesema ajali za barabarani kwa sehemu kubwa husababishwa na makosa ya kibinadamu wakiwemo wananchi wanaolewa na kutembea barabarani, madereva walevi pamoja na kuendesha vyombo vya moto kwa mwendo kasi makosa ambayo yamekuwa yakichangia kwa sehemu kubwa ajali hizo.
Baadhi ya watumiaji wa vyombo vya moto Mkoani hapa wakiwemo waendesha pikipiki maalufu kama bodaboda wamesema abiria wamekuwa ni kisababishi moja wapo cha kutokea kwa ajali hizo na hii ni kutokana na abiria wao kuwa na haraka kwa kuwataka kuongeza mwendo ili kufika mapema.
Hata hivyo baadhi ya wakazi wa mkoa wa dodoma akiwemo bw. mobara kishiwa pamoja na ashely Baraka wamesema madereva hawapaswi kutanguliza masilahi mbele na kukiuka sheria za usalama barabarani ikiwemo kwenda mwendo kasi kupakia abiria kupita kiasi na kusababisha ajali hizo.
Na Pis Jayunga Chanzo: Dodoma Fm Radio
Comments
Post a Comment