Licha
ya jamii kuendelea kuelimishwa juu ya kulinda watu mwenye ualbino wasiweze
kupata madhara yatokanayo na saratani ya ngozi bado swala hilo linaonekana kuto
kupatiwa kipaumbele katika baadhi ya maeneo.
Katibu
wa chama cha watu wenye ualbino Mkoa wa Dodoma Bwana Maiko Salali ameyasema hayo
wakati akizungumza na Dodoma FM habari juu ya mkakati uliopo ili kuwasaidia watu wenye
ualbino wasiweze kupata saratani ya ngozi kwa kuwaepusha na shughuli za juani.
Bwana
Salali amesema wakati jitihada hizo zikiendelea kufanyika wamekuwepo
baadhi ya walimu mashuleni ambao wamekuwa wakitoa adhabu kwa wanafunzi wenye ualbino na kusababisha wanafunzi hao kuwa hatarini kupatwa na saratani
ya ngozi.
Hata hivyo amebainisha kuwa Serikali kwa kushirikiana na uongozi wa watu wenye ualbino
Mkoani Dodoma wameanzisha Kliniki ya watu wenye ualbino ambapo wazazi pamoja
walezi wanapaswa kuwapeleka watoto wao ili kufanyiwa uchunguzi pamoja na
kupatiwa mafuta maalumu kwa ajili ya ngozi zao.
Na Pius Jayunga Chanzo: Dodoma Fm Radio
Comments
Post a Comment