JAMII IMETAKIWA KUTUMIA VYOO VYA KISASA
Na Dodoma fm
Wakazi wa maeneo ya vijijini mkoani Dodoma wameshauriwa kuacha kuendelea kutumia vyoo vya zamani na badala yake wajenge vyoo vya kisasa vinavyosafishika kwa urahisi ikiwa ni njia mojawapo ya kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.

Ushauri huo umetolewa na afisa afya wa
manispaa ya Dodoma Bwana Alek Saimon wakati akizungumza na kituo hiki ambapo
amesema katika maeneo ya vijijini bado wanajamii hawana elimu ya kutosha juu ya
ujenzi wa vyoo bora vya kisasa ambavyo ni rahisi kuvisafisha.
Bwana Alek amesema katika kuhakikisha
afya katika jamii inaendelea kuimarika manispaa ya Dodoma wanashirikiana na wadau mbalimbali katika ujenzi wa vyoo bora na
vya kisasa kwa gharama nafuu pamoja na utoaji wa elimu zitokanazo na matumizi
ya vyoo hivyo.
Hata hivyo amesema maeneo mengi vijijini
wanashirikiana na ngazi ya kata ambao ni
maafisa afya wa kata wanao pita kila nyumba kuhamasisha wananchi juu ya ujenzi
wa vyoo bora na vya kisasa.
Comments
Post a Comment