Skip to main content

BIASHARA


 TATIZO LA UKOSEFU WA ELIMU YA BIASHARA KWA VIJANA


Ukosefu wa elimu ya biashara imetajwa kama sababu ya vijana wengi  kuto kujishulisha na biashara yenye faida na manufaa. 

Akizungumza na kituo hiki mmoja wa vijana ambao wamejiajiri Francis Christopher amesema sababu mojawapo inayowarudisha nyuma vijana nikukosa Elimu yauzalishaji wa bidhaa pamoja na uendeshaji wa biashara jambo ambalo limekuwa likiwarudisha nyuma kimaendeleo.


Pamoja na hayo amesema vijana wanatakiwa kujitambua nakujua nini cha kufanya kwa wakati jambo ambalo linaweza kupunguza tatizo la ajira hususani kwa vijana.
clip kijana.



KUELEKEA SIKUKUU YA IDD BEI ZA BIDHAA SOKO KUU MAJENGO BADO ZAPANDA NA KUSHUKA.

Na Dodoma Fm

Wafanyabiashara wa Soko Kuu Majengo Mkoani Dodoma wamezungumzia hali ya biashara katika kuelekea msimu wa sikukuu ya idd mnamo mwezi September ikiwemo bidhaa kushuka na zingine kupanda hasa ukilinganisha na msimu wa bidhaa husika na kupelekea wateja kuwa wachache.

Wakizungumza na kituo hiki wafanyabiashara hao wamesema kuwa kulingana na maandalizi ya sikukuu hiyo bei za bidhaa zimetofautiana kutokana na msimu wa bidhaa husika ikiwemo viungo vya chakula kupanda na bidhaa nyingine kubaki bei yake ikiwemo nyama na mchele, na bidhaa zingine kushuka bei ikiwemo viazi na mahindi.

Bw. Khalid Ally amebainisha sababu mbalimbali za biashara sokoni hapo kuwa ngumu hasa kwa kipindi hiki cha kuelekea sikukuu ya idd kuwa ni pamoja na kukosekana kwa wanafunzi wa vyuo.

Bei za bidhaa katika msimu wa kuelekea sikukuu ya idd kwa sasa zimetegemea na msimu wa mazao yenyewe hivyo kila mwananchi ametakiwa kukabiliana na  hali ya bei ya bidhaa ambazo zimeonekana zikipanda na nyingine kushuka.
Chanzo: Dodoma FM.

Comments

Popular posts from this blog

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifug...

WAJAWAZITO WASHAURIWA KUTUMIA VIDONGE VYA FOLIC ACID KUEPUKA WATOTO VILEMA

                                                                  Mama wajawazito wameshuriwa kutumia dawa aina ya FOLIC ACID katika kipindi cha miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito ili kuepuka kupata mtoto mwenye   mapungufu. Rai hiyo imetolewa na Daktari kutoka Hospitali ya Matovyolwa mjini Dodoma   Dk.MUBARACK ISSA ALI wakati akizungumza na Dodoma FM juu ya athari zitokanazo na mama kutotumia dawa hizo. Dr Mubarack amesema katika kipindi cha ujauzito mama huwa anapitia changamoto nyingi hivyo ni vyema akatumia dawa aina ya FOLIC ACID ili kuepuka kupata mtoto mwenye tatizo la mgongo wazi, kichwa kikubwa pamoja na upungufu wa damu. Aidha Dk. Mubarack amesema   ili kuepuka kupata mtoto njiti   kipofu na kusababisha kifo kwa mtoto   ni vyema mama akaepuka matumizi ya pombe, dawa za kulev...

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madi...