Skip to main content

BURUDANI

 TWANGALA-KUPATA NAFASI BONGO MUVI NI KAZI

Msanii wa maigizo na bongo movie kutoka Dodoma Twangala amesema kupata fursa ya kuonyesha kipaji ulichonacho katika muvi ni kazi ngumu hivyo kupelekea watu kukata tama.


Amesema hayo wakati akizungumza na Beat Drive Show ya Dodoma fm ambapo amebainisha kuwa kuna watu wengi wanavipaji lakini kupata nafasi ni vigumu.


Akizungumzia kuhusu kupata fursa kwa upande wake amesema alianza katika matamasha mbalimbali ikiwepo katika tamasha la mtoto wa afrika ndipo baadae wakaunda kikundi cha maigizo.


Ameongeza kuwa jamii imekuwa ikiwachukulia waigizaji kama watu ambao hawataki kufanya kazi kitu ambacho sio kweli huku akisema kuna wasanii wengi ni maarufu na wana kipato cha juu.


Amemaliza kwa kuwataka wasanii kuwa na upendo na kuacha chuki binafsi hali inayoweza kupelekea kurudisha nyuma sanaa.


Miongoni mwa muvi alizofanya ni pamoja na Vanessa na mkono wa mungu


Na Beny Bert

 

GIFTED SON-MAMBO YALIKUWA MENGI,NDO MAANA NIMECHELEWA KUACHIA SHIDA  

Msanii wa mziki  wa Bongo fleva miondoko ya rap Gifted Son kutoka Dodoma ameeleza sababu zilizopelekea kuchelewa kwa video yake ya Shida kutoka kwenye albam yake ndogo ya shida.


Mwaka jana msanii huyo kutoka Biorn entertainment aliachia albam yake yenye nyimbo 5 ambayo inaenda kwa jina la shida.


Akizungumza na Beat Drive Show ya 98.4 Dodoma FM amesema video ya wimbo huoo imeandaliwa toka mwaka 2017 lakini walisimamisha zoezi la kuachia kazi hiyo kutokana na kazi mpya ambayo walipanga kuachia lakini mambo yaliingiliana.


Akizungumzia kuhusu nyimbo zingine ambazo hajatolewa video katika album hiyo amesema muda wowote anaweza akatoa kwa sababu anaamini bado ana muda wa kutosha.

Mwaka 2017 msanii huyo aliaachia album yake ndogo ambayo ilitajwa kuwa ni kazi iliyompa mpa sifa nzuri nje ya mipaka ya Tanzania ikiwepo Kenya Uganda mpaka nchi ya Zambia.


Na Beny Bert

 

ZIPORAH-JAMII YA KIAFRIKA HAIMPI NAFASI MWANAMKE

 



Msanii wa mziki wa kizazi kipya kutoka Dodoma Zipora ameilaumu jamii kutokana na kutoa nafasi kubwa kumsapoti mwanaume huku mwanamke akiachwa nyuma.

Ziporah ni ni miongoni mwa wasanii wa kike ambao wanatajwa mara nyingi kwa kuwa na kipaji cha mziki pamoja na sauti nzuri ya uimbaji.

Akizungumza na Beat Drive Show amesema jamii kubwa ya kiafrika inatoa nafasi kubwa kwa mwanaume bila kujua kuwa mwanamke ananafasi kubwa na anaweza kufanya zaidi ya kile ambacho mwanaume anaweza kufanya.

Akizungumzia kuhusu kuwepo kwa wasanii wachache wakike mkoani Dodoma amesema baadhi yao ni waoga na baada ya kufanya kazi chache hawaoni umuhimu wakuendelea kufanya kazi hiyo ili waendelee kuongeza ukubwa wa majina yao.

Hata hivyo ametoa ushauri kwa watayarishaji wa mziki mkoani Dodoma kutokuridhika hivyo kuongeza juhudi na jitihada ili waongeze ukubwa wa kazi zao.

Ameongeza kuwa kwa mwaka 2018 ana mikakti ya kuongeza ukubwa wa kazi zake ikiwa ni pamoja na kufanya kazi na watayarishaji wa mziki kutoka nje ya mkoa wa Dodoma.

Na Beny Bert


 

 MIRACLE NOUMA-KAZI YANGU IMEFANYA VIZURI 




Msanii wa mziki wa kizazi kipya kutoka Dodoma Miracle noma ameonesha kufurahishwa baada ya mapokezi mazuri ya kazi yake ambayo amemshirikisha Godzilla inayoenda kwa jina la ups and Down


Akizungumza na Dodoma fm amesema kazi yake imepokelewa vizuri kitu ambacho hakutegemea kama itakuwa hivyo


Akizungumzia kuhusu utofauti aliouona baada ya kumshirikisha Godzilla kwenye wimbo huo amesema ameongeza mashabiki wengi kutokana na msanii huyo kuwa na idadi kubwa ya watu wanaofatilia mziki wake


Hivi karibuni zilivuma tetesi huenda kundi ambalo yupo msanii huyo C.M.A limevunjika kutokana na muanzilishi wa kundi hilo Bin Laden kuwa bize na mambo yake kitu ambacho miracle amekataa sio kweli


Amemaliza kwa kusema kuwa wanasubiri kila mmoja atoe kazi yake kama solo artist ndipo kazi za kundi zitoke

Na Beny Bert   


FIDELIS-WAONGOZAJI WA VIDEO SIO WABUNIFU
 

 

Waongozaji wa video mkoani Dodoma wametakiwa kuwa wabunifu na kuongeza conection  ili kuleta ushindani wa video bora nchini na nje ya Tanzania.

 Fidelis ni miongoni mwa wasanii wa mziki wa kizazi kipya kutoka Dodoma amesema waongozaji wengi wa video hawathamini kazi za wasanii  kitu ambacho hakitakiwi katika sanaa ya bongo fleva.

 Amesema muongozaji anatakiwa amsaidie msanii kuweza kuongeza watu muhimu kitu ambacho kinahitaji nguvu kubwa.

 Hivi karibuni niliongea na moja kati ya waongozaji wa video Erick Backamaza ambaye amefanya kazi mbalimbali zikiwemo baadhi ya video za jacobeat alisema kwa waongozaji wapya wanaochipukia lazima wawe wabunifu ili kuvutia soko la mziki wa bongo fleva.
 

Miongoni mwa waongozaji wapya wanaofanya vizuri kutoka Dodoma ni pamoja na Nicklas ambaye ameshoot wimbo wa roma zimbabwe pamoja na mikono juu wimbo wa nay wa mitego.

 Na Beny Bert                                                         Chanzo Dodoma Fm 



YULE MKAKA-MSANII LAZIMA UJUE KUISOMA GAME INAHITAJI NINI

Image may contain: 1 person
Kutokana na kubadilika kwa sanaa ya mziki wa bongo fleva nchini wasanii wametakiwa kubadilika ikiwa ni pamoja na kuto kutoa  wimbo mara moja moja kwa kufanya hivyo itasaidia kukuza brand ya msanii.

Zamani ilikuwa ni vigumu kwa msanii kutoa wimbo kila baada ya mwezi mmoja lakini kwa kipindi hiki imekuwa ni jambo la kawaida katika tasnia ya mziki wa bongop fleva nchini.


Moja kati ya wasanii wanaofanya vizuri mkoani hapa Albert lakini jina lake la usanii ni YULE MKAKA amesema yeye ni miongoni mwa watu waliokuwa wakitoa kazi moja na kusubiri kwa muda flani lakini sasa hivi ameamua kubadilika hiyo ni baada ya kusoma game ya bongofleva inataka kitu gani.

Amesema mara nyingi amekuwa akitumia hashtagi ibebe dodoma hii ni baada ya kuamini kuwa Dodoma kuna vipaji vingi ila tatizo ni kuwa seriazi na kujiamini ambapo amemtaja moni centrozone kama icon ya mkoa na kila kitu inawezekana endapo wasanii hao watakuwa na juhudi binafsi.


Amemaliza kwa kuwataka mashabiki wote kukaa mkao wa kula ambapo mda sio mrefu anakuja na kazi nyingine 


Hivi karibuni Yule makaka ameachia kazi yake ambayo inaitwa kitochi. 


SAL-MO BIORN NI MIONGONI MWA LEBO ZINAZOFANYA VIZURI


Msanii na mtayarishaji wa mziki wakizazi kipya Salmoo kutoka more feelings production amesema baadhi ya lebo zilizopo mkoani hapa zina msaada mkubwa kwa wasanii kwani kuna utofauti mkubwa kwa sasa ukitofautisha na zamani.

Salmoo amesema hayo wakti akizungumza na Dodoama Fm Radio ambapo ameitaja lebo ya biorn kuwa ni miongoni mwa lebo inayowasimamia wasanii vizuri.

Akizungumzia kuhusu ukuaji wake katika kutayarisha mziki amesema kumechangiwa na producer mwenzake melodies ambaye amehusika kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo amesema msanii hutakiwi kutegemea kufanya staili moja ya mziki ila unatakiwa kuwa kila upande.


Hivi karibuni msanii huyo ameachia kazi yake mpya inayoitwa my wife aliyomshirikisha jacobeat ambapo amesema anafanya utaratibu wa kushoot video hadi kufika mwezi wa tatu itakuwa tayari.

Na Beny Bert                              
 

KISS MASTER : ZAIDI YA LAKI 5 NIMEZITUMIA -KWENYE VIDEO YANGU

Msanii  ambae anachipukia katika sanaa ya bongo fleva kutoka Dodoma kiss master amesema wakati anashoot video ya wimbo wake mr ngada alikuwa anakutana na changamot mbalimbali hali iliyokuwa ikimkatisha  tama ya kushoot video hiyo.


Kiss master amesema hayo wakati akizungumza na Dodoma Fm ambapo amesema changamoto hizo zilikuwa zikimkatisha tama lakini alijitaahidi kadri ya uwezo wake ili afanikiwe zoezi hilo.


Akizungumzia juu ya gharama ambazo ametumia katika kushoot video ya wimbo wake mr ngada amesema ametumia zaidi ya laki 5 licha ya kutokuwa na uongongozi unaomsimamia.


Amesema baada ya kuachia video ya mr. ngada aliyomshirikisha tasha ladiva kuna kazi nyingine ambayo inakuja aliyo mshirikisha god zilla.


Hadi sasa kazi hiyo ina viwers 812 katika mtandao wa yotube toka iachiwe wiki moja iliyopita.


Na Beny Bert     

Comments

Popular posts from this blog

MITI YA KIVULI MAARUFU KAMA PANGA UZAZI YAZUA TAHARUKI WILAYANI BAHI DODOMA

                                                  Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bahi Jijini Dodoma Dk.Philipina Philipo amewatoa hofu wakazi   wa Wilaya hiyo juu ya taarifa za kuwepo kwa madhara katika miti ya kivuli maarufu kama PANGA UZAZI ambayo imezua hofu kwa wananchi hao. Hoja hiyo imeibuliwa katika kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri hiyo ambapo baadhi ya madiwani wameomba kupatiwa ufafanuzi kuhusu kuwepo kwa fununu kuwa mti huo una madhara na kuongeza kuwa baadhi ya wananchi wameanza kuikata wakihofia kupatwa na madhara hayo. Akitoa ufafanuzi kuhusu miti hiyo Mganga Mkuu wa Wilaya Dk.Philipina Philipo amesema hadi hivi sasa hakuna utafiti wowote uliofanyika na kubainisha kuwa mti huo hauna madhara hivyo wananchi hawana haja ya kuhofia chochote. Kutokana na Majibu hayo ya DK PHILIPINA yamepelekea kuibua kwa hoja nyingine kwa madiwani ambapo baadhi yao wametoa maoni tofauti tofauti juu ya ufafanuzi huo. Kufuatia hayo katibu  tawala msaidizi mkoa anayesh

YANGA KESHO KUJUA ANACHEZA NA NANI KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

MAJINA ya vigogo wa soka Afrika, wakiwemo mabingwa wa Afrika 1998, Raja Casablanca yametawala katika orodha ya wapinzani wapya wa Yanga kwenye michuano ya Afrika. Yanga SC imeangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, ambako watamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo. Hiyo ni baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya sare ya 0-0 na wenyeji, Township Rollers Jumamosi jioni Uwanja wa Taifa mjini Gaborone nchini Botswana. Matokeo hayo yanamaanisha Rollers inakwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza historia hiyo kwa ushindi wa jumla wa 2-1 uliotokana na matokeo ya mchezo wa                              kwanza Dar es Salaam Machi 6. Na Yanga SC itamenyana na moja ya timu zilizofuzu hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo, ambazo ni CR Belouizdad, USM Alger za Algeria, Al-Masry ya Misri, Djoliba ya Mali, Raja Casablanca, Enyimba ya Nigeria, SuperSport United ya Afrika K

MIKOA INAYOONGOZA KWA UKEKETAJI TANZANIA YATAJWA

Mila potofu   katika jamii ya kimasai imetajwa kuwa changamoto kwa maafisa ustawi wa jamii wa halimashauri ya wilaya ya Ngorongoro  kutokana na kukosa ushirikiano wa kutatua Tatizo la ukeketaji kwa jamii hiyo. Akizungumza na waandishi ya habari Afisa Ustawi Wa jamii Bwana ALOYCE  LOLIKISWALI katika semina iliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu Sanyansi na Utamaduni UNESCO kwa lengo la kupinga ukeketaji wa wanawake amesema kukosekana kwa ushirikiano kwa jamii imekuwa ni changamoto ambayo imepelekea kushindwa kudhibiti ukeketaji pamoja na ukatili wa kijinsia. Kwa upande wake Mwenyekiti wa Malaigwanan Bwana JOSEPH TIRIPAI amebainisha kuwa mila na desturi zao zitabadilika kulingana na wakati lakini watahakikisha wanalinda watoto wanaozaliwa kutokeketwa na kusisitiza elimu kuendelea kutolewa hususani shuleni. Katika hatua nyingine mratibu wa afya ya mama na mtoto ameeleza kuwa wanawake wajawazito waliokeketwa wanalazimika   kujifugua kwa upasuaji na